Heshima anayopewa mkongwe Kelvin Yondani na wachezaji wenzake katika kikosi cha Yanga inadhihirisha umuhimu wake katika timu hiyo
Baada ya kuondoka Ibrahim Ajib, wachezaji waandamizi wa Yanga wametaka kitambaa hicho akabidhiwe Yondani
Kocha Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kufanya uamuzi hata hivyo ni dhahiri jukumu hilo atapewa Yondani kwa kuwa ndiye chaguo la wachezaji wenzake
Katika kikosi cha sasa cha Yanga, Yondani na Juma Abdul ndio wachezaji ambao wamedumu kwa muda mrefu zaidi
Yondani ameitumikia Yanga kwa miaka saba, akijiunga na mabingwa hao wa kihistoria mwaka 2012 akitokea klabu ya Simba
Katika kipindi chote alichoitumikia Yanga, Yondani amekuwa akijitoa sana
Yondani alishirikiana vizuri na Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye kwa sasa ni Meneja wa Yanga baada ya kustaafu
Mwanzoni mwa msimu alikabidhiwa jukumu la unahodha kabla Zahera hajamuondolea wadhifa huo na kumkabidhi Ajib