Wachezaji wa kigeni Yanga wapata vibali vya kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jul 2019
Wachezaji wa kigeni Yanga wapata vibali vya kazi

Uongozi wa Yanga msimu huu umefanikiwa kukamilisha kwa wakati kupatikana kwa vibali vya wachezaji wake wote wa kigeni hivyo kuwa na uhakika wa kuweza kuwatumia kwenye michuano mbalimbali

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amethibitisha kuwa wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa a Yanga vibali vyao vimekamilika

Yanga imesahihisha makosa yaliyotokea msimu uliopita ambapo kocha Mwinyi Zahera hakuweza kukaa kwenye benchi la Yanga kwa karibu miezi mitatu kutokana na kutokamilika kwa vibali vyake

Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa na Yanga ni Farouq Shikalo, Lamine Moro, Mustapha Suleyman, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Juma Balinya na Sadney Urikhob

Wote wako kambini Morogoro isipokuwa Shikalo ambaye atatua nchini mwishoni mwa wiki

Naye kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki akitokea mapumzikoni nchini Ufaransa

Zahera alikwenda mapumziko baada ya kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo kwenye michuano ya Afcon 2019 timu hiyo ikitolewa hatua ya 16 bora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
33m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
58m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’