Kikosi cha Yanga kesho Ijumaa, Julai 19 kitacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Moro Kids ikiwa ni sehemu ya program ya mazoezi ya timu hiyo
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu hiyo imekusudia kucheza michezo mitano ya kirafiki katika maandalizi yake yanayoendelea mkoani Morogoro
Mapema wiki hii, Yanga ilicheza na Tanzanite Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 10-1
Kwenye mchezo huo Yanga huenda ikawakosa nyota wake Lamine Moro na Maybin Kalengo ambao walishindwa kufanya mazoezi leo kutokana na sababu mbalimbali
Moro anasumbuliwa na Malaria wakati Kalengo amepata majeraha ya kifundo cha mguu
Kalengo pia hakucheza mchezo dhidi ya Tanzanite Fc kutokana na majeraha hayo
ADVERTISE HERE