Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limevikumbusha vilabu vya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili kuwa ni siku 10 tu zimebakia kabla ya dirisha la usajili nchini Tanzania kufungwa
TFF imesisitiza hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya dirisha hilo kufungwa Julai 31 2019

Wakati huohuo, awamu ya pili ya dirisha la usajili wa michuano ya CAF linafungwa leo
Baada ya dirisha kufungwa leo, kuanzia kesho hadi Julai 31 timu zitaruhusiwa kusajili kwa kulipa faini ya dola 500 kwa kila mchezaji lakini wachezaji hao watakaosajiliwa wataruhusiwa kucheza kuanzia hatua ya makundi
ADVERTISE HERE