Baada ya Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kutoa ratiba ya michezo ya awali michuano ya ligi ya mabingwa, klabu ya AS Vita itaanzia ugenini nchini Cameroon kucheza na USM De Loum
Mchezo huo utapigwa sawa na ule wa Yanga dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa kati ya August 09, 10 na 11
Hivyo vigogo hao wa soka kutoka DR Congo hawana uwezekano wa kuja Tanzania August 04 kisha kuelekea Cameroon
Kwa upande wa Yanga, hakutakuwa na changamoto kwa kuwa mchezo wao wa kwanza utaanzia nyumbani
Uongozi wa Yanga leo utazungumza na waandishi wa habari, pengine inaweza kutangaza timu nyingine ambayo watacheza nayo August 04 kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi
ADVERTISE HERE