Winga Mrisho Ngasa ni mchezaji mwenye furaha sana kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa
Baada ya 'majembe' kadhaa kutua kikosini, Ngasa amenufaika na ujio wa mafundi hao kwani kwa kiasi kikubwa wamemfanya kuwa bora zaidi
August 04 Yanga imepanga kutambulisha kikosi chake siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi kwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki
Hata hivyo mabingwa hao wa kihistoria watalazimika kusaka timu nyingine ya kujipima nayo baada ya AS Vita kusitisha mpango wa kuja kutokana na kubanwa na ratiba
Sasa Ngasa anapendekeza waletwe hata hao majirani wa Msimbazi tuwaonyeshe kazi mapema tu
Winga huyo 'teleza' anaamini Yanga imeiva na iko tayari kukabiliana na timu yoyote ndani au nje ya nchi
Bahati mbaya Simba nao wataanzia ugenini michuano ya ligi ya mabingwa hivyo sababu yao itakuwa kama ya AS Vita
Uongozi wa Yanga uko kwenye mchakato wa kusaka timu mbadala wa AS Vita ambayo itakuja nchini kunogesha kileleni cha wiki ya Mwananchi, August 04, uwanja wa Taifa