Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul bado hajaonekana kwenye mazoezi ya timu hiyo mkoani Morogoro sambamba na mabeki Kelvin Yondani na Andrew Vicent
Hata hivyo, Abdul amekanusha taarifa zinazodai kuwa amegomea kuingia kambini akishinikiza amaliziwe fedha za usajili
"Taarifa za mimi kugoma hazina ukweli wowote, nina matatizo ya kifamilia, muda sio mrefu mtaniona kikosini," amesema
Abdul ni miongoni mwa wachezaji walioongeza mikataba kuendelea kukipiga Jangwani baada ya mikataba ya awali kumalizika
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kwani hakupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ubora wa Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye kiwango chake cha msimu uliopita kimemfanya aitwe timu ya Taifa inayojiandaa kucheza na Kenya Julai 28
Kutofanya mazoezi ya mwanzo wa msimu kunaweza kumuweka Abdul katika wakati mgumu zaidi wa kupata namba kutokana na usajili uliofanywa na Yanga
Kwa nyakati tofauti kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amemtumia beki Ally Ally nafasi ya ulinzi wa kulia wakati huu ambao Boxer yuko kwenye kikosi cha Stars
Yanga imeongeza walinzi wanne kwenye kikosi chake wakiongozwa na Mghana Lamine Moro, Ally Mtoni, Ally Ally na Mustapha Suleyman