Wiki ya Mwananchi inatarajiwa kuanza rasmi Jumapili ya Julai 28 2019
Katika wiki hiyo ambayo itahitimishwa August 04, Wanayanga watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yanayo wazunguuka
Yanga ni timu ya Mwananchi, kuthibitisha hilo, Wanayanga watatumia wiki nzima kufanya mambo mema kwenye jamii zao
Watajitolea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kufanya usafi, kuchangia damu mahospitalini, kusaidia jamii zenye mahitaji muhimu n.k
Zoezi hilo litahitimishwa uwanja wa Taifa August 04 kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kupigwa
Siku hiyo burudani mbalimbali zitakuwepo uwanja wa Taifa lakini kubwa zaidi ni utambulisho wa kikosi cha Yanga pamoja na utambulisho wa jezi za msimu wa 2019/20
Hili litakuwa tukio la kihistoria, kwa hakika inafaa kila Mwanayanga akajiandaa kuwa sehemu ya historia hiyo itakayoandikwa uwanja wa Taifa August 04