Uongozi wa klabu ya Yanga umesema wiki ya Mwananchi itazinduliwa rasmi visiwani Zanzibar Jumamosi Julai 27 2019
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa Kamati ya Hamasa Deo Mutta amesema tukio hilo litaanzia jijini Dar es salaam asubuhi na jioni msafara wa Yanga utaelekea visiwani Zanzibar kwa ajli ya uzinduzi
Mutta amesema wameamua kuzindua wiki ya Mwananchi visiwani Zanzibar ili kumuenzi Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa klabu ya Yanga
Miongoni wa shughuli zitakazofanyika visiwani Zanzibar ni pamoja na kuzulu kaburi la hayati Karume lililoko Kisiwandui
Wiki ya Mwananchi itazinduliwa uwanja wa Amaan, ukumbi wa Judo
ADVERTISE HERE