Kelvin Yondani amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom. Yeye pamoja na Andrew Vicent 'Dante' wamecheza michezo yote minne.
Katika mchezo wa juzi dhidi ya Ndanda ambapo Yanga iliondoka na ushindi wa bao 1-0, Yondani ndiye aliyetoa majaro iliyozaa bao la Yanga lililofungwa na Ibrahim Ajib.
Uwezo wake wa kuzuia pia kupanda mbele kuongeza mashambulizi kila anapopata nafasi ni moja ya mambo yanayomfanya atofautiane na walinzi wengine wa kati.
Juzi kocha George Lwandamina baada ya mchezo dhidi ya Ndanda hakusita kumwagia sifa Yondani na kusema kwake ndiye aliyekuwa 'Man of the Match'.
Yondani ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga walioitwa na Salum Mayanga, kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania kuunda kikosi cha Stars ambapo kitacheza na Malawi Oktoba 07 kwenye mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA.

ADVERTISE HERE