Serikali imesema Sheria ya uwekezaji kwenye timu za mpira wa miguu nchini iliyoruhusu wawekezaji kupewa hisa asilimia 49 na Wanachama asilimia 51, hairuhusu mwekezaji mmoja kuhodhi hisa zote asilimia 49
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema sheria hiyo inataka wawekezaji waanzie watatu na kuendelea
Waziri Mwakyembe amesema Sheria hiyo haikusimamiwa ipasavyo na TFF hivyo Serikali imeanza mchakato wa kutunga kanuni na marekebisho ambapo zoezi hilo litasimamiwa na BMT
"Hairuhusiwi mwekezaji mmoja kuhodhi asilimia 49, mchakato ulipoanza tuliwambia TFF wasimamie ipasavyo, lakini hawakufanya hivyo," Dk Mwakyembe aliwaambia waandishi wa habari
"Hivyo tumeanza mchakato wa kanuni ya marekebisho na mchakato huo utafanya na BMT na si TFF"