Uongozi wa klabu ya Yanga leo umezindua rasmi wiki ya Mwananchi ambayo itahitimishwa August 04 kwa mchezo mkali wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kariobangi Sharks kupigwa kwenye uwanja wa Taifa
Jijini Dar es salaam maadhimisho hayo yamezinduliwa Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani ambapo wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo wamejitokeza kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alizindua maadhimisho hayo kwa kupanda mti sambamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Yanga Princess Suzan Massawe
Baadae burudani zaidi zitahamia Mbagala Zakheim
Kesho msafara wa viongozi wa Yanga utaelekea visiwani Zanzibar kuzindua maadhimisho hayo
ADVERTISE HERE