Kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, ya Tanzania Bara, George Lwandamina, amesema anajivunia ubora wa kikosi chake licha ya kuonyesha kiwango cha chini katika mechi nne za ligi.
Kwenye mahojiano na mtanadao wa GOAL, Lwandamina amesema bado anaijenga Yanga yake kwa kuwaingiza kwenye mfumo wachezaji aliowasajili kuziba mapengo yaliyoachwa na wachezaji walioondoka.
"Niseme ukweli sina hofu yoyote ya kupoteza kibarua changu kwasababu kazi ninayoifanya inakwenda vizuri na hata matokeo tunayoyapata siyo mabaya kwani tupo nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara Mtibwa Sugar"
"Kushindwa kuonyesha kiwango cha kuvutia na kufunga mabao machache nijambo la mpito ambalo linasababishwa na mchanganyiko uliopo unahitaji muda kidogo wachezaji kuzoeana ili waanze kufanya kile ambacho mashabiki wanakitaka kukiona,"amesema Lwandamina.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema idadi ya wachezaji walioondoka ni kubwa na mbaya wote walikuwa wakicheza kikosi cha kwanza hivyo isingekuwa rahisi kiasi hicho wachezaji wapya kuziba kwa haraka mapengo yao kutokana na mabadiliko ya mifumo kutoka huko walipokuwa kuja Yanga.
Amesema ukiacha Papy Tshishimbi ambaye ameweza kukopi kwa haraka, wachezaji wengine wameanza taratibu na kadri muda unavyokwenda ameanza kuona mabadiliko jambo ambalo linampa imani ya kufanya vizuri.
Yanga imeshinda michezo miwili , kati ya minne ambayo wamecheza msimu huu, na kufikisha pointi nane huku ikiwa na wastani wa kufunga bao moja katika kila mechi.

ADVERTISE HERE