Uongozi wa klabu ya Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya GSM kesho Augudt 02 wanatarajiwa kuzindua jezi za timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2019/20
Tukio hilo litafanyika Hoteli ya Kempinski jijini Dar es salaam
Kampuni ya GSM ambayo ilishinda zabuni ya kutengeneza na kusambaza vifaa vya Yanga, ndio itakayosimamia mauzo ya jezi na habari njema jezi hizo zitapatikana nchi nzima
Inaelezwa baada ya uzinduzi huo, jezi zitaanza kuuzwa kuelekea August 04 siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi
ADVERTISE HERE