Jumapili August 04, kunako dimba la Taifa kuna historia nyingine itaandikwa kwa mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi
Siku hiyo ni maalum kwa Wanayanga kutambulishwa timu yao, jezi na baadae kushuhudia mchezo wa kukata na shoka kati ya Yanga dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya
Lakini mapema kutakuwa na matukio mengine ya burudani
Mechi mbili za kukata na shoka zitapigwa. Ya kwanza itawahusisha wasanii wa Bongo Muvi dhidi ya wenzao wa Bongo Fleva (Team Kiba vs Team Kigosi)
Baadae mchezo mwingine wa kihistoria utapigwa, mchezo huo utawahusishwa wakongwe waliotamba vilabu vya Yanga na Pamba Fc kuanzia miaka ya 70
Kwa wale vijana wenzangu ambao hatukuwahi kupata nafasi ya kuwashuhudia wazee wetu wakisakata kabumbu, basi tutawaona
Pia wengi tunawasikia majina tu na historia zao, lakini siku hiyo itakuwa nafasi nzuri kuwafahamu
Uongozi wa Yanga umepanga kuwa jezi zitakazotumiwa na wakongwe hao zitaandikwa majina yao mgongoni
