Uongozi wa klabu ya Yanga umesema jezi mpya za klabu hiyo zitaendelea kupatikana baada ya kumaliza changamoto zilizojitokeza
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema upo mzigo wa jezi za kutosha, changamoto ziliyojitokeza zinahusiana zaidi na masuala ya kiutendaji
Amesema mauzo ya jezi yatarejea wakati wowote katika vituo vilivyotangazwa
Yanga ilizindua jezi jana, lakini muda mfupi baadae, jezi hizo ziliadimika madukani baada ya mashabiki kuzinunua zote zilizokuwa sokoni
ADVERTISE HERE