Mshambuliaji mpya wa Yanga David Molinga leo amejumuika na wachezaji wa timu hiyo katika mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Uhuru
Molinga aliyesajiliwa na Yanga juzi, amefanya mazoezi leo chini ya usimamizi wa kocha Mkuu Mwinyi Zahera
Mshambuliaji huyo hakupata nafasi ya kuingia kambini mkoani Morogoro baada ya usajili wake kuchelewa

Lakini bila shaka atakuwa tayari kuwakabili Kariobangi Sharks kesho
ADVERTISE HERE