GSM yamwaga mzigo zaidi wa jezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2019
GSM yamwaga mzigo zaidi wa jezi

Baada ya hapo jana kutokea sintofahamu kufuatia kumalizika kwa jezi mpya za Yanga muda mfupi baada ya uzinduzi, kampuni ya GSM imewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa jezi zitaendelea kupatikana kwa wingi

Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa jezi ambapo leo umati wa mashabiki ulifurika Makao Makuu ya Yanga na katika maduka ya GSM kununua jezi ambazo hata hivyo upatikanaji wake ulikuwa wa kusuasua

Meneja Masoko wa kampuni ya GSM Hersi Said amesema wanaendelea kusambaza jezi za kutosha katika maeneo yote ya mauzo

"Mzigo upo ila ulimalizika kwenye maeneo ambayo tulipeleka lakini limefanyiwa kazi na jezi zitapatikana, si hivyo tu kuna mzigo mwingine unaingia kwa kila ndege inayokuja kutoka China kwani hatukuweza kusafirisha kwa pamoja kutokana na muda pamoja na gharama za usafirishaji," amesema

"Niwatoe hofu mashabiki wa Yanga kuhusu hilo, jezi watazipata ingawa hatukutarajia kama muitikio ungekuwa mkubwa namna hii, inaonyesha ni kiasi gani Yanga ina mashabiki wengi kutokana na mahitaji kuwa makubwa"

"Hizi jezi zinazouzwa ziliingia juzi (Alhamisi) usiku na pia tarehe ya uzinduzi na kilele cha Wiki ya Wananchi nazo zimekuwa karibu sana, hivyo hata usafirishaji ukawa changamoto kidogo ingawa hilo halizuii upatikanaji wa jezi mpya za Yanga"

Hadi kufikia mchana wa leo, jezi zilianza kupatikana kwenye maduka yote ya GSM

Jezi hizo pia zitapatikana kesho Uwanja wa Taifa kwenye vituo maalum vya mauzo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’