Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kariobangi Sharks, umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
Baada ya shamrashamra za wiki ya Mwananchi zilizodumu kwa takribani siku saba, zimehitimishwa kwa mchezo huo kupigwa katika dimba la Taifa baada ya shughuli ya kutambulisha kikosi cha Yanga
Yanga ikiwa na nyota wengi wapya, ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza ambapo ilitengeneza nafasi nyingi lakini washambuliaji wake Sadney Urikhob, Patrick Sibomana na Juma Balinya walishindwa kuzitumia
Katika kipindi cha pili, Kariobangi walirejea wakiwa imara zaidi na walitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 48 likiwekwa kimiani kwa shuti kali na Patrick Otieno
Patrick Sibomana aliisawazishia Yanga bao hilo kwenye dakika ya 57 kupitia mkwaju wa penati ambao ulitolewa na mwamuzi Elly Sassie baada ya mlinzi wa Sharks kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu hata hivyo hakuna timu iliyoweza kuongeza bao
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alitumia mchezo huo kukipima kikosi chake ambacho wiki ijayo kitaikabili Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa
Alifanya mabadiliko ya wachezaji watatu tu Juma Balinya, Sadney Urikhob na Mohammed Issa 'Banka' ambao nafasi zao zilichukuliwa na Maybin Kalengo, Mrisho Ngasa na David Molinga