Yanga kujichimbia Zenji kujiandaa na ligi ya mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2019
Yanga kujichimbia Zenji kujiandaa na ligi ya mabingwa

Kikosi cha Yanga, kinatarajiwa kusafiri keshokutwa Jumatano mchana kuelekea Zanzibar ambako wataweka kambi ya siku mbili kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers

Yanga inatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, Agosti 10 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema timu yao itasafiri Jumatano mchana kuelekea Zanzibar ambako watacheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam, Ijumaa.

Ten amesema wakiwa visiwani humo, wataanza kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mlandege FC siku ya Jumatano kisha watacheza na Malindi, Alhamisi.

"Tunaamini mwalimu ataendelea kukijenga kikosi chetu ili tufanye vizuri, Jumamosi, tunachoomba Wazanzibar waipokee timu yao, nilivutiwa na vile ambavyo mashabiki wa Yanga walijitokeza taifa, " amesema.

Ten amesema viingilio kwenye mchezo wa Jumamosi ni 5,000 kwa mzunguko huku VIP ikiwa 15,000 na lile eneo maalum zaidi ikiwa 50, 000.

"Yanga imerudi kwenye zama zake hivyo ni jukumu letu kujitokeza kwa wingi Jumamosi ili kuisapoti, kipindi kile tuliteleza hivyo hatutegemei kurudia makosa ya awamu ile," amesema.

Yanga wanakumbukumbu ya kuondolewa mwaka jana na Township Rollers wakiwa chini ya George Lwandamina aliyetimkia ZESCO United, kwa jumla ya mabao 2-1.

Matokeo hayo yalipatikana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa, Machi 6 jijini Dar es Salaam walipoenda Botswana walitoka suluhu, Machi 17 ndani ya mwaka huo.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’