Moja ya habari kubwa leo ni kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya DR Congo Florent Ibenge ambaye pia ameachia ngazi kuinoa AS Vita
Kuachia ngazi kwa kocha huyo kunaweza kuwa habari nzuri kwa Yanga kwani Mwinyi Zahera Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria, alikuwa akimsaidia kuinoa timu ya Taifa
Kujiuzulu kwake kunamaanisha kuwa huenda akaondoka na benchi lake la ufundi ambalo lilikuwa likiundwa na yeye, Zahera na Mihayo Kazembe kocha wa TP Mazembe
Majukumu ya timu ya Taifa yalimchelewa Zahera kujiunga na kambi ya Yanga mkoani Morogoro
Pengine huu ni wakati mzuri kwa viongozi wa Yanga kuzungumza na Zahera ili abaki na majukumu ya kuinoa Yanga tu
Β
ADVERTISE HERE