Mashabiki Yanga watavunja rekodi ya mwaka 2016?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2019
Mashabiki Yanga watavunja rekodi ya mwaka 2016?

Keshokutwa Jumamosi, August 10 2019 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na Township Rollers katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali

Mchezo huo utapigwa saa 12 jioni

Baada ya kuujaza uwanja wa Taifa Jumapili katika tukio la kilele cha wiki ya Mwananchi, kwa mzuka walionao mashabiki, hali inaweza kujirudia Jumamosi

Yanga inahitaji sana sapoti ya mashabiki wake ili kupata ushindi mnono kwenye mchezo huo wa nyumbani

Wingi wa mashabiki uwanjani ni silaha muhimu katika vita ya kusaka ushindi nyumbani

Miaka mitatu iliyopita, ikishiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, Yanga iliweka rekodi ya kuujaza uwanja wa Taifa mapema kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo uliopigwa Juni 28 2016 na Yanga kufungwa bao 1-0, mageti ya uwanja wa Taifa yalifungwa saa nane ambapo Jeshi la Polisi likilazimika kufanya kazi ya ziada kuwaondoa mashabiki wengi waliobaki nje

Licha ya kupoteza mchezo, Yanga ilikuwa bora na wingi wa mashabiki ulinogesha mtanange huo

Jumamosi ni nafasi nyingine kwa Wanayanga kudhihirisha kuwa jina la 'Wa Kimataifa' hawakupewa kwa bahati mbaya

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’