Yanga kurejea na dawa ya Rollers leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2019
Yanga kurejea na dawa ya Rollers leo

Kikosi cha Yanga kimemaliza maandalizi ya siku tatu visiwani Zanzibar na kinarejea leo tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers hatua ya awali

Kesho Jumamosi August 10, mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa saa 12 jioni mbele ya mashabiki wake

Kocha Mkuu Mwinyi Zahera alitaka timu yake ipate michezo zaidi ya kirafiki kabla ya kuikabili Rollers

Lengo la Zahera lilikuwa kupata muunganiko wa kikosi chake ambacho kina maingizo mapya mengi

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Malindi uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Zahera alisema kwa kiasi kikubwa timu yake imeiva, na ana matumaini makubwa watafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho

"Tupo Sawa, tulikuwa na changamoto ya muunganiko wa kikosi, naamini msimu huu tutafanya vizuri kwenye ligi kuu na ligi ya mabingwa," amesema

Aidha kupitia michezo hiyo ya kirafiki, Zahera amesema amepata kikosi chake cha kwanza

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’