Ettiene Ndayiragije ndiye kocha wa Mbao FC tangu msimu uliopita. Bado ana mkataba wa muda mrefu na timu hiyo.
Siku chache zilizopita kumeibuka taarifa kuwa klabu ya Yanga imemtaka kocha huyo achukue nafasi ya Shedrack Nsajigwa ambaye huenda akarejesha kwenye majukumu yake ya kikosi cha Yanga B.
Taarifa hizo zimekanushwa vikali na viongozi wa Yanga hata Mbao imesisitiza kuwa kocha huyu bado ana mkataba wa muda mrefu na haina mpango wa kumuachia aondoke.
Taarifa za chinichini zimebainisha kuwa ni kweli Yanga imewasiliana na kocha huyo na mazungumzo baina ya pande mbili bado 'hayajafa'.
Inadaiwa Ndayiragije amekuwa mzito kukubali nafasi ya msaidizi wa Lwandamina anataka awe kocha Mkuu.
Meck Mexime kocha wa Kagera Sugar ni miongoni mwa makocha waliowahi kufuatwa na Yanga ambaye naye aligoma kuwa kocha msaidizi.
Yanga inahitaji kuimarisha benchi lake la Ufundi na sasa inasaka kocha mahiri atakayeweza kusaidiana na Lwandamina katika kuisuka klabu hiyo inayokabiliwa na michuano ya Kimataifa miezi michache ijayo.

ADVERTISE HERE