Yanga yasaka ushindi dhidi ya Township Rollers leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Aug 2019
Yanga yasaka ushindi dhidi ya Township Rollers leo

Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo wanarejea rasmi katika majukumu ya Kimataifa kwa kumenyana na Township Rollers katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali

Mchezo huo wa kwanza utapigwa dimba la Taifa kuanzia saa 12 jioni

Viingilio vya mchezo; VIP A Tsh 50,000/- VIP B na C Tsh 15,000/- Mzunguuko Tsh 5,000/-

Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga iliyorejea katika michuano ya CAF baada ya kukosa kwa msimu mmoja

Mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuipa sapoti Yanga ambayo itakuwa ikiwakilisha nchi

Yanga inahitaji kuibuka na ushindi leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza

Uwepo wa mashabiki wengi uwanjani, utawahamasisha wachezaji kuipigania timu iweze kupata ushindi

Aidha huu ni mchezo wa kisasi kwa Yanga kwani ni hawahawa Rollers ambao waliwaondosha kwenye michuano ya ligi ya mabingwa mwaka jana

Wakati Yanga ikishuka uwanja wa Taifa, watani zao Simba watakuwa dimbani huko Msumbiji kuumana na UD Songo

Mchezo wa Simba utaanza mapema zaidi ambapo itakuwa ni saa 11 jioni kwa saa za Tanzania

KMC nayo itakuwa uwanjani huko Rwanda ikicheza na AS Kigali katika mchezo wa kombe la Shirikisho

Azam Fc itashuka dimbani kesho Jumapili nchini Ethiopita kuumana na Fasil Ketema

Ni muhimu kwa wawakilishi wote wa Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano ya CAF mwaka huu ili kuendelea kujihakikishia ushiriki wa nafasi nne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
26m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’