Uongozi wa Yanga huenda ukafanya mabadiliko katika kitengo chake cha habari ambapo Mwanahabari Antonio Nugaz huenda akamrithi Dismas Ten
Nugaz amekuwa akisimamia matukio makubwa yote ya klabu ya Yanga akiwa 'MC'
Aidha Ten ambaye sasa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, huenda akarithi moja kwa moja nafasi hiyo iliyoachwa na Charles Boniface Mkwasa
Kumekuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wanataka mabadiliko kwenye kitengo hicho kutokana na kukosekana kwa hamasa
Siku ya tukio la Kubwa Kuliko, Rais Mstaafu awamu ya nne Mh Dk Jakaya Kikwete alishangazwa na kutokuwepo kwa hamasa miongoni mwa mashabiki wa Yanga kujitokeza uwanjani tofauti na watani zao Simba
Hali hiyo imejitokeza juzi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambapo mashabiki wachache walijitokeza uwanjani
Wengi wanadhani hakuna hamasa ya kutosha ya kuwafanya mashabiki watoke majumbani kwao kuelekea uwanjani