Fei Toto apania kurudi kikosi cha kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Aug 2019
Fei Toto apania kurudi kikosi cha kwanza Yanga

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum amesema kukosa kwake nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers kunamfanya ajitathimini ni wapi anakosea.

Yanga iliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Township Rollers kwenye uwanja wa nyumbani na wanatarajia kuwafuata wapinzani wao kwaajili ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 20 hadi 23.

Fei Toto alisema nafasi yake katika kikosi cha kwanza inachangamoto kubwa kutokana na usajili uliofanyika kila mchezaji anatakiwa kupambana mwenyewe kuhakikisha anajitengenezea mazingira ya kupata namba kikosi cha kwanza.

"Nimeona makosa kidogo kwa wenzangu na hiyo ndio itakayokuwa njia ya mimi kuyafanyia kazi na kuonyesha mazoezini ili niweze kurudi kikosini na naamini hilo linawezekana."

"Kuona mapungufu yao haina maana kwamba hawakucheza inavyotakiwa walicheza vizuri, lakini kuna vitu walitakiwa kuviongeza ili timu iweze kupata matokeo hivyo nimeshaanza kuvifanyia kazi ili niweze kupata nafasi ya kucheza mchezo wa marudiano," alisema Fei Toto.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’