Kiungo Abdulaziz Makame 'Bui' amesema mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ulikuwa ni mazoezi mazuri kwao kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Bui amewataka mashabiki wa Yanga wasiumizwe na matokeo waliyopata kwenye mchezo huo kwani yalikuwa ni mazoezi tu
"Mashabiki wetu inapaswa waelewe mchezo wa soka una matokeo matatu, sisi tumepata moja ya matokeo hayo"
"Lakini pia wanafahamu huu ulikuwa mchezo wa mazoezi tu, ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya ligi ya mabingwa"
"Matokeo tuliyopata leo hayamaanishi kuwa tutapoteza mchezo wetu dhidi ya Rollers"
Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Polisi Tanzania katika mcheo uliopigwa uwanja wa Chuo cha Ushirika, Moshi
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Yanga kucheza wilayani Moshi baada ya kupita miaka 16