Tusiipime Yanga kwa mechi ya kirafiki - Muro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2019
Tusiipime Yanga kwa mechi ya kirafiki - Muro

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro ambaye amewahi kuwa Msemaji wa klabu ya Yanga, amesema mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania hauwezi kutumika kama kipimo cha uimara wa Yanga

Muro ambaye alikuwepo uwanjani jana kushuhudia mchezo huo ambao Yanga ilifungwa kwa mabao 2-0, alisema matokeo hayo hayakuwafurahisha mashabiki lakini sio kipimo sahihi cha uimara wa timu yao

"Uimara wa Yanga haupimwi kwenye mechi za kirafiki. Tuipime Yanga kwenye mechi za Kimataifa kwa mfano sasa tuko kwenye michuano ya ligi ya mabingwa tunajiandaa kwenda Botswana," amesema

"Tukitoka Botswana tunakuja kuanza ligi, tuipime Yanga kule"

"Yanga ni timu yetu, hii kupoteza leo na Polisi ndio tumeumia lakini tusiipime Yanga hapa"

"Tusimpime Mwalimu hapa"

Hata hivyo Muro ameeleza kutofurahishwa na uamuzi wa kocha Mwinyi Zahera kutowapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao mashabiki wengi walifika uwanja wa Chuo cha Ushiriki kuwaona

"Mashabiki wa Yanga wanataka raha, wanataka furaha sasa ni vyema uongozi wa Yanga ukaliangalia hili"

"Hapa mashabiki walikuja kwa wingi uwanjani kuwaona wachezaji wanaowapenda lakini hawakuwepo"

"Hatujawaona akina Ngasa, Tshishimbi na wengineo.."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’