Jezi Yanga kupatikana kwa urahisi zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2019
Jezi Yanga kupatikana kwa urahisi zaidi

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema awamu ya tatu ya shehena ya jezi za Yanga inatarajiwa kuwasili wakati wowote ambapo kutakuwa na mabadiliko ya bei ya jezi hizo

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Yanga Kaloleni jijini Arusha leo, Dk Msolla amesema kutakuwa na punguzo la bei ili kuwawezesha mashabiki na wanachama kununua kufuatana na uwezo wao

"Zile jezi tulizozindua kwenye awamu ya kwanza zilikuwa toleo daraja la juu ambazo zilikuwa za wachezaji na ziliuzwa Tsh 35,000/- na baadae likaletwa toleo la mashabiki ambazo ziliuzwa Tsh 30,000/-"

"Tulizungumza na GSM na tukakubaliana, jezi za awamu ijayo, lile toleo la juu zitauzwa kwa Tsh 30,000/- na zile za mashabiki zitauzwa Tsh 20,000/-"

"Lengo ni kuwawezesha mashabiki na wanachama wetu kununua jezi kwa kulingana na uwezo wao"

Aidha Dk Msolla amesema ujio wa jezi hizo utamaliza changamoto ya kukosekana kwa jezi mpya za Yanga madukani

Kampuni ya GSM imeahidi kuwezesha upatikanaji wa jezi za Yanga nchi nzima

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’