Yanga yaomba sapoti ya Watanzania Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2019
Yanga yaomba sapoti ya Watanzania Botswana

Kuelekea mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi ugenini dhidi ya Township Rollers, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amewatoa hofu mashabiki kuhusu kupata matokeo, huku uongozi ukiomba sapoti kubwa kutoka kwa Watanzania waishio Botswana.

Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela, aliliambia gazeti la Nipashe kuwa, wameanza kufanya mazoezi kwenye uwanja ambao watautumia siku ya mechi na wachezaji wote wana ari kubwa ya ushindi.

"Tayari tumeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi, lengo ni kuhakikisha tunavuka hatua hii na kuweza kusonga mbele," alisema na kuongeza kuwa jana mchana walifanya mazungumzo na Watanzania waliopo nchini humo, kwa lengo la kupanga mikakati ya ushindi.

Alisema kocha Zahera amesema anataka kufika mbali katika michuano hiyo licha ya kuwa na ushindani mkubwa.

"Zahera amesema atahakikisha tunarudi na matokeo mazuri nyumbani kikubwa anaomba dua za Watanzania"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’