Wadau mbalimbali wameendelea kujitolea kumwaga kifusi eneo la uwanja wa Yanga, Kaunda Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani
Zoezi hilo liko kwenye hatua za mwisho ambapo likikamilika, matengenezo ya sehemu ya kuchezea 'pitch' yataanza
Kwa kuanzia, uwanja huo unatatandikwa nyasi bandia
Uongozi wa Yanga uliandaa mpango wa miezi mitatu kukamilisha matengenezo ya uwanja huo
Makamu Mwenyekiti Yanga Fredrick Mwakalebela alisema wamepanga kuutumia uwanja wa Kaunda msimu huu
"Kwa sasa tutakarabati sehemu ya kuchezea, ni zoezi ambalo litachukua takribani miezi mitatu"
"Lengo letu ni kuhakikisha msimu huu tunakuwa na uwanja wetu wa mazoezi ili kupunguza gharama"
"Gharama tunazotumia kukodi viwanja ni kubwa, pesa hiyo inaweza kutusaidia katika masuala mengine"
Aidha, Kuhusu adha ya mafuriko Jangwani, Mwakalebela amesema kifusi kilichowekwa kimepunguza adha hiyo ambapo wadau wanaendelea kuongeza kifusi ili kuondoa kabisa tatizo hilo