Inaelezwa idadi kubwa ya waandishi wa habari nchini Botswana wamekuwa wakifika kwenye uwanja ambao Yanga inafanya mazoezi hali iliyopelekea uongozi kupiga marufuku mtu asiyehusika kuingia kuwashuhudia
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimetoa malalamiko kuwa Yanga inawazuia kutimiza majukumu yao
Hata hivyo uongozi umesisitiza kuwa kwa sasa sio wakati wa waandishi wa habari kufanya mahojiano na wachezaji au viongozi
Presha imekuwa kubwa kuelekea mchezo huo ambapo wengi wameonekana kuihofia Yanga kutokana na kiwango walichoonyesha kwenye mchezo wa kwanza
Aidha Rollers wanadaiwa kupenyeza watu wao kwa kupitia kofia ya uandishi ili kuchunguza kinachofanywa na Yanga
Kitendo cha Yanga kuwasili mapema nchini Botswana kimewashtua kwani wametambua ni kiasi gani Yanga imedhamiria kushinda mchezo huo