Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limekataa maombi ya mabadiliko ya uwanja yaliyopelekwa na Township Rollers
Rollers walitaka kuupeleka mchezo wa Jumamosi kwenye uwanja mdogo ambao CAF wameukataa kwa kuwa haukidhi vigezo
Hivyo mchezo wa marudiano kati ya Township Rollers dhidi ya Yanga utapigwa kwenye uwanja wa Taifa wa Botswana ambao ukubwa wake unakaribiana na uwanja wa Mkapa hapa Tanzania
Inaelezwa kukataliwa kwa mabadiliko hayo kumewavuruga mabosi wa Rollers ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika michezo mingi waliyocheza kwenye uwanja huo mdogo, wenyewe wanapaita 'machinjioni'
Uamuzi huo wa CAF ni habari njema kwa Yanga kwani sasa watacheza kwenye uwanja sawa na huu wa Taifa ambao waliutumia kwenye mchezo wa kwanza
ADVERTISE HERE