Rollers watumia pombe kuwaita mashabiki uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2019
Rollers watumia pombe kuwaita mashabiki uwanjani

Mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Township Rollers dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi August 24 uwanja wa Taifa, Botswana umeendelea kuwa gumzo

Baada ya Yanga kuwasili mapema nchini Botwana huku wakijifua chini ya ulinzi mkali kukwepa hujuma, inaelezwa Rollers wameingia mchecheto ambapo sasa wamekimbilia kwa mashabiki wao kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi kuwapa nguvu keshokutwa

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wao wa Taifa baada ya CAF kugoma kuupeleka kwenye uwanja mdogo ambao Rollers huwa wanautumia

Sasa Rollers wamekuja na mpango wa kuwashawishi mashabiki kuujaza uwanja huo wa Taifa

Licha ya kuweka viingilio vidogo (Kiingilio cha juu ni Tsh 10,000/- na cha chini ni Tsh 2,000/-), Rollers wameahidi uwanjani kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na pombe!

"Katika mchezo huo Jumamosi hii, mbali ya soka la kiwango cha juu na la kuvutia, pia kutakuwa na burudani ya muziki na pombe za ‘kumwaga’ uwanjani," ilisomeka taarifa ya kuwahamasisha mashabiki iliyotolewa na Rollers

Mshindi wa mchezo huo atajihakikishia kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa

Yanga inahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili wakati Rollers wanahitaji ushindi au suluhu ya bila kufungana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’