Kiungo wa Opara United inayoshiriki ligi kuu ya Botswana, Mtanzania Abdallah Hamis leo aliwatembelea wachezaji wa Yanga ambao kesho watashuka dimba la Taifa la Botswana kuikabili Township Rollers
Hamis ambaye asili yake ni Mwanza, alikutana na 'nduguze' Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa wanaotokea Mwanza pia
Kiungo huyo mkabaji aliyeitumikia timu ya Taifa mara kadhaa wakati akicheza Kenya, ameiunga mkono Yanga na ana matumaini kesho itaibuka na ushindi dhidi ya Rollers
ADVERTISE HERE