Yanga leo inakabiliwa na mchezo muhimu wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa uwanja wa Taifa huko Botswana
Ili kuhakikisha timu yake leo inatumbukiza mabao, kocha Mwinyi Zahera wiki nzima alikuwa akijaribu mifumo tofauti ya uchezaji
Leo Zahera anaweza akatumia kikosi kilichocheza mechi dhidi ya AFC Leopards na kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki, ambapo mfumo wa 4-4-2 unaweza kutumika

Lakini pia kwa nyakati tofauti kwenye mazoezi, kocha Zahera alimjumuisha kiungo Feisal Salum kwenye kikosi cha kwanza na kufanya awe na viungo watatu wa kati pamoja na washambuliaji watatu
Hivyo upo uwezekano pia leo akamuanzisha Fei Toto akacheza kiungo akichukua nafasi ya Sadney na kumuacha Balinya akiwa mshambuliaji pekee wa kati huku Balama na Sibomana wakiungana nae wakitokea pembeni

Mfumo huu utaisaidia Yanga kuwa na namba kubwa katikati hivyo kuwa na uhakika wa kumiliki mpira. Viungo hao pia watakuwa wakienda kushambulia na kurudi kuzuia pale timu inapopoteza mpira