Hatuwahofii ZESCO United - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2019
Hatuwahofii ZESCO United - Dk Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema baada ya kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, sasa wanajipanga kuikabili ZESCO United

Akizungumza usiku wa kuamkia leo kwenye mapokezi ya kikosi cha Yanga uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dk Msolla amesema anaamini Yanga ina nafasi ya kupata ushindi dhidi ya ZECO na kutinga hatua ya makundi

"Kama Mwalimu atafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na wachezaji kutambua umuhimu wa mchezo huo, nadhani tutapita," amesema

"Hatumhofii kocha George Lwandamina kwani kwa sasa hatufahamu, tuna timu mpya"

"Labda ni mchezaji mmoja au wawili ambao aliwafundisha ndio wapo"

"Hata Kamusoko aliyeondoka hapa juzi, akija atashangaa kwani atakutana na sura za wachezaji wengi ambao hawafahamu"

Dk Msolla amesema Yanga ina malengo ya kufika mbali kwenye michuano hiyo

Na hata ikitokea bahati mbaya wakatolewa, watakuwa na nafasi nyingine kwenye michuano ya kombe la Shirikisho

Kikosi cha Yanga kimewasili usiku wa kuamkia leo kikitokea Botswana ambako kilifanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa Township Rollers bao 1-0

Licha ya kuwasili usiku sana, mashabiki walijitokeza kwenye mapokezi ya mashujaa hao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’