Baada ya kumaliza majukumu ya Kimataifa, timu za KMC na Azam Fc leo zitashuka kwenye uwanja wa Uhuru kumenyana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa kwanza
Mabingwa wa kihistoria Yanga wao watakuwa dimbani kesho Jumatano kuchuana na Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru
Alhamisi itakuwa zamu ya Simba kushuka kwenye uwanja wa huo ikiwa mgeni wa JKT Tanzania
Baada ya kukamilika kwa michezo ya raundi ya kwanza ligi inatarajiwa kusimama kwa takribani wiki mbili kupisha michezo ya kalenda ya FIFA
ADVERTISE HERE