Baada ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, kesho Jumatano kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Uhuru kucheza mchezo wake wa kwanza ligi kuu ya Vodacom
Hesabu za kocha Mwinyi Zahera ni kuhakikisha Yanga inaanza kampeni yake ya kusaka ubingwa wa ligi kuu kwa ushindi
Wachezaji walipata mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka Botswana na leo wanafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo
Yanga imeweka kambi Hoteli ya Nefaland jijini Dar es salaam
Katika moja ya mahojiano yake, Zahera alisema msimu huu utakuwa wa furaha kwa Wanayanga kwani wana timu imara
Matumaini ya ushindi kuelekea mchezo huo ni makubwa, ari ya wachezaji iko juu kutokana na mafanikio waliyopata Botswana
ADVERTISE HERE