Wachezaji Paulo Godfrey 'Boxer' na Mohammed Issa 'Banka' wataukosa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa kesho kwenye uwanja wa Uhuru
Daktari wa kikosi cha Yanga Dk Edward Bavu, amethibitisha wachezaji hao kuwa majeruhi
Boxer alipata maumivu ya nyama za paja kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers wakati Banka aliumia kabla ya mchezo wa Rollers lakini alilazimika kucheza mchezo huo
Dk Bavu amesema beki Ally Ally aliyepata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania, amepona na amerejea kikosini
ADVERTISE HERE