Tshishimbi atamba, timu imeiva

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2019
Tshishimbi atamba, timu imeiva

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema kikosi chao kimeanza kuchanganya baada ya wachezaji kuzoeana

Yanga iliwasili usiku wa kuamkia jana kutoka Botswana ambako ilitinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa Township Rollers bao 1-0

Tshishimbi amesema mechi za kirafiki walizocheza pamoja na michezo miwili dhidi ya Township Rollers, imesaidia kuwaunganisha

Mcongomani huyo amesema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi huku wakipiga hesabu ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa

"Mwanzo tulikuwa hatuchezi vizuri kwa sababu wachezaji wengi wapya, hatujazoeana," amesema

"Lakini michezo tuliyocheza imetusaidia, tutafanya vizuri zaidi kadiri tunavyoendelea kucheza pamoja"

Aidha kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Tshishimbi amesema watapambana kupata matokeo ili kuwapa furaha mashabiki pamoja na kutimiza malengo ya timu msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
29m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
37m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’