Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amewapa ujumbe wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga kuwa hakuna njia ya mkato kupata mafanikio.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, kocha huyo mpole asiye na maneno mengi ameandika ujumbe ambao ni dhahiri unawalenga wale waliokata tamaa na mwenendo klabu ya Yanga msimu huu.
MANENO YAKE
"The most beautiful people we have known are those who have known defeat, known suffering, known struggle, known loss, and have found their way out of the depths. These persons have an appreciation, a sensitivity, and an understanding of life that fills them with compassion, gentleness, and a deep loving concern. Beautiful people do not just happen," Lwandamina
TAFSIRI ISIYO RASMI
"Watu waliofanikiwa ni wale waliopitia kwenye machungu ya aina mbalimbali. Kuna wakati walishindwa, wakaumizwa na kupoteza matumaini. Lakini hawakukata tamaa, wakajituma na wakafanikiwa.
"Watu hawa wana shukrani, wapole, wakarimu na wanaelewa maisha yaliyowajaza ukarimu, upole na upendo. Watu hawa hawatokei tu" imesomeka sehemu ya ujumbe wa Lwandamina uliotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.
Yanga inapita katika kipindi kigumu sasa nje na ndani ya uwanja ambapo kwa ujumbe huo ni dhahiri Lwandamina anawataka wadau wa klabu hiyo wawe na tabia kama za watu waliofanikiwa.

ADVERTISE HERE