Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla leo alialikwa kwenye Mkutano wa viongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam
Kwenye Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Dk Msolla aliwataka viongozi hao kuwa na umoja na kushirikiana ili kuhakikisha Yanga inafanya vizuri msimu huu
"Jambo muhimu ni umoja, itakuwa ngumu kwetu viongozi kuongoza timu ambayo wanachama na mashabiki wake wamegawanyika," amesema
"Tunahitaji matokeo mazuri msimu huu ili kuyapata ni lazima tuwe wamoja"
ADVERTISE HERE