Nitavaa mavazi wanayotaka - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2019
Nitavaa mavazi wanayotaka - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema atalipa faini aliyotozwa kutokana na mavazi aliyovaa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Aidha, ameongeza pia kuwa atavaa kama walivyotaka

Jana Kamati ya Bodi ya ligi ilitangaza kumtoza Zahera faini ya Tsh 500,000/- kutokana na kuvaa mavazi ambayo hayana staha ndani ya uwanja walipocheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting

Hata hivyo Zahera amesisitiza kuwa bado haielewi kanuni hiyo kwani haoni tatizo la mavazi yake aliyotumia August 28

"Mimi nipo tayari kulipa, lakini nashangazwa na kanuni hizi maana ukiangalia nilivaa pensi ndefu ambayo ina heshima," amesema

"Siwezi kukataa sababu wameamua, sasa hivi nitakuwa ninavaa mavazi wanayoyataka, nguo ninazo nyingi"

Pamoja na adhabu hiyo, Zahera pia alifungiwa mechi tatu akidaiwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’