Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga wako jijini Mwanza wakijifua kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Mchezo huo wa kwanza utapigwa Septemba 14 uwanja wa Taifa kisha timu hizo kurudiana baada ya wiki mbili
Ili kuhakikisha timu inafanikisha kutinga hatua ya makundi, uongozi wa Yanga umewaahidi wachezaji donge nono kama watavuka kizingiti cha ZESCO United
Wachezaji wa Yanga walizawadiwa Tsh Milioni 50 baada ya kuiondoa Township Rollers katika hatua ya awali
Sasa inaelezwa dau hilo litaongezwa mara tatu kama wataiondoa ZESCO United na kutinga makundi
Kocha Mwinyi Zahera amesema wamepania kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu
ADVERTISE HERE