Jumamosi ya Septemba 14 2019, mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga watashuka dimba la Taifa kuikabili ZESCO United katika mchezo wa kwanza, raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga ndio muwakilishi pekee wa Tanzania aliyebaki kwenye michuano hiyo baada ya watani zao Simba kutolewa mapema tu, hatua ya awali
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema Septemba 14 ni siku muhimu kwa Wanayanga, amewataka wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa
Yanga ina dakika 180 za kupata ushindi dhidi ya ZESCO na kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa
Kwa kutinga makundi tu, Yanga itajihakikishia sio chini ya Tsh Bilioni moja
ADVERTISE HERE