Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema anaamini kama Mcongomani Heritier Makambo angekuwepo Yanga, timu zingeteseka sana
Hafidh amemsifu Makambo kuwa ni mshambuliaji aliyefahamu kufunga na kazi yake aliyoifanya Yanga ilionekana japo alicheza kwa msimu mmoja tu
"Yanga imesajili nyota wengi wa kigeni ambao walikuwa bora na waliisaidia timu kufikia malengo wakiwemo kina Hamis Kiiza, David Mwape, Kenneth Asamoah na wengine wengi kila mmoja anakumbukwa kwa mazuri yake, lakini kwa Makambo ameondoka kipindi ambacho timu bado inamuhitaji," Hafidh amenukuliwa na Mwanaspoti
"Makambo alikuwa mpambanaji na hakubali kushindwa hadi dakika za mwisho. Kipindi hiki bado timu imekosa mtu kama yeye kutokana na kushindwa kupata matokeo jambo ambalo naamini ni la muda tu"
Makambo aliuzwa klabu ya Horoya AC kwa dau linalokaribia Tsh Milioni 180 na Yanga kusajili safu mpya ya ushambuliaji yenye nyota kama David Molinga, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Maybin Kalengo na Patrick Sibomana
Hata hivyo kasi ya upachikaji mabao bado hairidhishi hivyo kuwapa hofu mashabiki wa Yanga ambao wana shauku kubwa kuiona timu yao ikifanya vizuri msimu huu
Hata hivyo Hafidh amesema suala hilo ni la muda tu, baada ya wachezaji hao kucheza pamoja kwa muda na kuzoeana, watafunga