Timu zinatukamia - Dante

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2017
Timu zinatukamia - Dante
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga ilibanwa nyumbani na Mtibwa Sugar na kutoka suluhu, ikiwa ni mechi ya pili nyumbani kushindwa kutoka na ushindi msimu huu, lakini beki wake wa kati Andrew Vincent 'Dante' amefichua siri ya suluhu hiyo.

Yanga ilirudi Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya mechi tatu za ugenini Nyanda za Juu Kusini, tangu walipolazimishwa sare ya 1-1 na wageni wa Ligi Kuu msimu huu, Lipuli Iringa, lakini Mtibwa wakawabania tena.

Dante aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Mtibwa, alisema matokeo ambayo Yanga imekuwa inakumbana nayo msimu huu ni rekodi za ubingwa walizonazo ambazo zimefanya timu pinzani kucheza nao kwa umakini mkubwa.

Alisema timu zimekuwa zikicheza kwa umakini ili kuepuka kuaibika mbele ya Yanga na kutolea mfano mechi ya juzi namna Mtibwa alivyocheza kwa utulivu na kuokoa kila aina ya shambulio kali langoni mwao na matokeo kuwa yalivyokuwa.

Yanga imeanza msimu huu kwa kasi ndogo ikishinda mechi mbili tu kati ya tano ilizocheza mpaka sasa, jambo ambalo limeibua hali ya wasiwasi kwa mashabiki wao lakini Dante anasema rekodi ya kutwaa ubingwa mara tatu ndiyo tatizo.

"Lazima jambo hili likae akilini mwa mashabiki wa Yanga, sio kila timu inafurahia mafanikio ya Yanga ya kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo, nadhani ni wakati wa kusaka mbinu mpya ili tuweze kutimiza malengo yetu," alisema Dante.

"Nimeona kwenye mechi kama tatu hivi jinsi ambavyo wapinzani wetu wametukamia kana kwamba soka sio burudani, hilo lazima lituamshe na kuangalia namna nyingine ya kukabiliana na wapinzani wetu," alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
40m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’