Yanga yapinga Zahera kufungiwa mechi tatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2019
Yanga yapinga Zahera kufungiwa mechi tatu

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ukipinga uamuzi wa Bodi ya Ligi kumfungia kocha Mwinyi Zahera mechi tatu kutokana na shutuma za upendeleo alizotoa kwa Bodi hiyo baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting

Katika mchezo huo wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu, Zahera alilalamikia hatua ya Bodi ya Ligi kukataa kusogeza mbele kwa siku mbili mechi dhidi ya Ruvu Shooting hasa ikizingatiwa Yanga ilipaswa kusafiri kutoka Botswana

Yanga ilicheza Botswana August 24 na ikasafiri kurejea nchini usiku wa kuamkia August 26, wachezaji wakipumzika siku moja tu kabla ya kushuka tena dimbani

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema adhabu ya kumfungia kocha mechi tatu ni kubwa pengine faini ingetosha

Pamoja na adhabu hiyo, Zahera alipigwa faini ya kulipa laki tano kutokana na mavazi aliyovaa kwenye mchezo huo

Hata hivyo wengi wameshangazwa na uamuzi huo kwani pamoja na adhabu kumkumba yeye, kocha msaidizi wa Ruvu Shooting nae hakuwa na mavazi rasmi lakini hakuadhibiwa

Mwakalebela amesema hawaoni kama Bodi ya ligi imemtendea haki Zahera

"Unapomfungia kocha mechi tatu kwa nini usimpe faini tu aendelee kufundisha timu?," amehoji Mwakalebela

"Tumeshaiandika barua Wizara kulalamikia haya madhaifu na tunasubiri majibu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’